SHINDA NA SIMACCOUNT

Zaidi ya 200 Tsh Milioni Kushindaniwa

Shindano letu ni rahisi sana kushiriki. Mshiriki anachotakiwa kufanya, ni kupiga *150*62# ambapo atakaribishwa kujiunga na SimAccount na kisha atachagua lugha. Baada ya hapo, mshiriki atasoma vigezo na masharti ya SimAccount na kuchagua kujisajili. Mshiriki atatakiwa kuweka namba ya siri na kuithibitisha kwa kuirudia tena. Baada ya hapo, mshiriki atapokea ujumbe mfupi kwenye namba yake ambayo itakuwa namba yake ya akaunti yaani SIMAccount, baada ya hapo, akaunti ya mteja itakuwa imesajiliwa usajili wa awali. Ili kuingia kwenye kinyang'anyiro cha za zawadi za kila wiki, kila mwezi, na katika droo kuu. Washiriki pekee waliokamilisha USAJILI ndio watakuwa na nafasi ya kushinda.

Ili mshiriki aweze kuingia kwenye droo ya kushinda, anatakiwa kukamilisha usajili wake kwa kutembelea tawi la CRDB Benki lililo karibu au wakala wa Fahari Huduma, punde baada ya kukamilisha usajili, mteja ataingia kwenye shindano moja kwa moja.

Kujiongezea nafasi zaidi za kushinda, mshiriki anatakiwa kufanya miamala ya huduma za SIMAccount. Kila muamala, utamuongezea mshiriki nafasi ya kushinda, mfano Usajili, kuweka fedha(amana) kwenye SimAccount, akiba, & kulipia bidhaa na huduma kwa SIMAccount.