CRDB Sim_0

Benki ya CRDB yaja na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi

Akizungumza jijini Dar es Salaam mapema wiki hii wakati wa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu huduma mpya kwa njia ya simu ya mkononi-SimAccount, Meneja wa huduma kwa wateja, Idara ya huduma za fedha kwa njia ya mtandao wa Benki ya CRDB, Edith Metta alisema huduma mpya ya SimAccount inawawezesha wateja kufungua akaunti ya kikundi, akaunti ya akiba na kununua bidhaa au kufanya ankara za malipo.

"Huduma hii inamuwezesha mteja kufanya manunuzi kwa njia ya simu kwa wafanyabiashara wote wanaopokea malipo kwa SimAccount "LIPA HAPA KWA SIMACCOUNT","Metta aliwaambia waandishi wa habari. Alisema kuwa kupitia mfumo huu mpya wa SimAccount, vikundi vinavyotaka kufungua akaunti havihitaji kutembela tawi la Benki ili kufungua akaunti. Kikundi, kupitia simu ya mkononi kinaweza kufungua akaunti na kuiendesha kwa uwazi, salama na rahisi. Wanakikundi wataweza kuona salio la akaunti ya kikundi kwa uwazi, fedha za kikundi hazitatoka kwenye akaunti ya kikundi bila ridhaa ya wanakikundi. SimAccount inawawezesha wanakikundi kupiga kura kuamua jambo lolote linalohusu fedha za kikundi zilizohifadhiwa kwenye akaunti ya kikundi.

Soma zaidi: https://www.ippmedia.com/en/news/crdb-bank-introduces-digital-package-solutions-market

Tags: hakuna vitambulisho

Acha maoni