Habari na Matukio

SimAccount ni nini?

SIMAccount ni mfumo wa kielektroniki ambao unamuwezesha mteja kujisajili na kufungua akaunti KUPITIA SIMU YA MKONONI na kupata huduma za kifedha kwa urahisi na salama. Mteja hahitaji kuwa na akaunti ya Benki kwanza ili kujisajili, bali mteja anatakiwa kuwa na simu tu ya mkononi, na namba ya simu iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi..

Inafanyaje kazi?

Mteja anatakiwa kupiga *150*62# na kufuata utaratibu wa usajili kisha kutembelea tawi lolote la Benki ya CRDB au wakala wa Fahari Huduma na kitambulisho kimojawapo kati ya KADI YA MPIGA KURA, KITAMBULISHO CHA TAIFA, LESENI YA UDEREVA au HATI YA KUSAFIRIA ili kukamilisha usajili.

Kumbuka: Wateja walio na SIMBanking watapata usajili wa kudumu mara moja.

Kwanini SimAccount?

AKAUNTI ZA VIKUNDI

SimAccount inawawezesha wateja kufungua akaunti maalum kwa ajili ya vikundi kwa madhumuni mbalimbali.

Vikundi hivi vimewezeshwa kufungua, kufuatilia na kusimamia akaunti ya kikundi kwa uwazi zaidi kwa wanachama wote wa kundi.

AKIBA

SIMAccount inamuwezesha mteja kufungua akaunti binafsi ya akiba na amana.

ANKARA ZA MALIPO

SimAccount inawawezesha wateja kulipa ankara mbalimbali ikiwemo maji, ving'amuzi, kununua umeme nk, na kulipia bidhaa mbalimbali kwa wafanyabiashara walio na huduma ya "LIPA KWA SIIMACCOUNT" walionea nchi nzima.

Nani anaweza kutumia SimAccount

Mtu yeyote aliye na simu ya mkononi yenye namba ya Tigo, Vodacom, Halotel na Airtel iliyosajiliwa kikamilifu anaweza kufungua SIMAccount.

Piga *150*62# na kisha fuata maelekezo kufanya usajili wa awali wa akaunti yako.
Usajili wa awali unakuwezesha kuona orodha ya baadhi ya huduma mbalimbali za SIMAccount. Hata hivyo, ili kuweza kufanya miamala ya fedha na kutumia huduma zote za SIMAccount, unatakiwa kukamilisha usajili wa akaunti yako.

Tembelea tawi la Benki ya CRDB lililo karibu yako, Vituo vya Huduma za Kibenki vya CRDB, au Mawakala wa Fahari Huduma na Kitambulisho chako(KADI YA MPIGA KURA, KITAMBULISHO CHA TAIFA, LESENI YA UDEREVA au HATI YA SAFARI) ili kukamilisha usajili wa akaunti yako. Utajaza fomu, kupiga picha na kisha taarifa zako zitachukuliwa kielektroniki na hivyo usajili wako kukamilika na hatimaye kukuwezesha kuanza kutumia huduma zote za SIMAccount.

Namba yako ya Simu uliyoisajili na SimAccount, ndio Namba yako ya Akaunti

Mteja anaweza kuweka fedha kwenye akaunti yake kwa kutembelea tawi lolote la Benki ya CRDB lililo karibu, kwa wakala wa FAHARI HUDUMA na Wakala wa SIMAccount , Fahari Huduma mawakala na SimAccount Agents nchini kote. Ukitembea tawi la Benki ya CRDB, utatakiwa kujaza fomu kuweka fedha na kuwasilisha fomu hiyo kwa Afisa wa Benki kwa kwa ajili ya kuweka fedha zako kwenye SIMAccount

Mitandao ya Kijamii

Tunapatikana kwenye kurasa za mitandao ya Kijamii