untitled (25 of 27)

CRDB waja na bidhaa tatu mpya, wizi wa pesa za vikoba kuwa historia!

Kufuatia matukio ya kukosekana kwa uaminifu kwa wanavikundi wanaowekeza pesa ili kujikwamua kiuchumi, benki ya CRDB imekuja na bidhaa tatu mpya kwa wateja wake ikiwamo wenye vikundi vya vikoba kupata akaunti kupitia simu zao za mkononi ili kuondokana na changamoto ambazo zinawakabili.

Meneja wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao wa benki hiyo, Edith Metta.

Meneja wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao wa benki hiyo, Edith Metta, ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusiana na huduma hizo mpya kwa wateja.

Alizitaja huduma hizo kuwa ni akaunti ya kikundi, akaunti ya akiba na akaunti ya malipo.

Metta alisema kumekuwa na changamoto katika baadhi ya vikundi vya fedha ikiwamo vikoba za kupotea kwa fedha au mmoja kukimbia nazo hivyo wameamua kuja na suluhisho kwa vikundi ili fedha zao ziwe salama.

Alisema wanachama wanauwezo wa kufungua akaunti ya pamoja kupitia simu zao za mkononi na kisha kusajili jina la kikundi na kuanza kuweka fedha pamoja na kutoa bila kuwepo na makato.

“Mwanachama wa kikundi ana uwezo wa kuangalia kiasi cha salio kilichopo katika akaunti ya kikundi na endapo kuna fedha imetolewa kinyemela wanajua kwa wakati na kuepusha mwanachama kukimbia na fedha ama kuambiwa fedha imeibiwa,” alisema

 

Read more: http://bongo5.com/crdb-waja-na-bidhaa-tatu-mpya-wizi-wa-pesa-za-vikoba-kuwa-historia-09-2018/

Tags: No tags

Leave a Comment